Manchester United tayari wanafikiria kuchukua nafasi ya Antony baada ya kuanza maisha vibaya Old Trafford, huku kikosi cha Erik ten Hag kikiwa na mpango wa kumnunua mchezaji wa zamani wa Real Madrid Takefusa Kubo badala yake.
Antony ametatizika kukidhi bei yake tangu uhamisho wake wa Euro milioni 95 msimu uliopita, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akishindwa kutoa bao au kusaidia katika mechi 18 msimu huu. Fowadi huyo amefunga mabao nane pekee na asisti tatu katika mechi 62 katika michuano yote na Ten Hag amethibitisha kuwa mwaminifu kwa nyota wake wa zamani wa Ajax, hata hivyo uvumilivu wa United unaonekana kupungua.
United wametuma maskauti kumtazama Kubo kwa Real Sociedad kwa angalau mara saba msimu huu, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 akiwa katika kiwango cha kuvutia kwa upande wa La Liga. Kubo amefunga mabao sita na asisti tatu katika mechi 14 alizoanza Sociedad mwaka huu, ametoa mchango wa mabao 13 msimu uliopita baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea Real kwa Euro milioni 6.5. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Japan ana mkataba hadi 2027 na Soceidad lakini kuna tetesi kuwa kuna kipengele cha kutolewa chenye thamani ya takriban €60m katika mkataba wake, ingawa Madrid pia wanaaminika kuwa na kipengele cha kumnunua tena kwa nusu ya kiasi hicho.