Jeshi la Ukraine limesema vikosi vyake vya ardhini vinaendelea kukabiliana na mashambulizi ya Urusi licha ya baridi kali na kwamba hapo jana wamefanikiwa kuzima jumla ya mashambulizi ya urusi 64.
Rais Volodymyr Zelensky amesema wanahitaji kuongeza kasi ya usambazaji wa vifaa kama droni kwa wapiganaji walio katika mstari wa mbele wUkraine inafikiria kuhamasisha watu 500,000 zaidi wajiunge na jeshi katika vita vyake na Urusia vita huku akikiri kuwa wanajeshi wake wanakabiliwa na uhaba wa risasi.
Leo Jumatano, wajumbe wa Baraza la pamoja la Jumuiya ya kujihami NATO na Ukraine watakutana mjini Brussels nchini Ubelgiji ili kujadili ongezeko la hivi karibuni la mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine ambayo yamesababisha vifo vya makumi ya watu.