Kampeni ya Ukarimu wa Vodacom kutoka Vodacom Tanzania Foundation inaendelea kusambaa Tanzania nzima wakati huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na mara hii umepokelewa kwa furaha na Wakazi wa Kanda ya Pwani.
Kampeni ya Ukarimu wa Vodacom kwa lengo la ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku imewafikia Watanzania wa Tanga katika maeneo ya Nyako, Mtindiro, Kwabeda na Korogwe Mjini.
Watanzania wa Mtwara nao wamefikiwa na Ukarimu wa Vodacom katika Wilaya ya Newala huku Lindi Ukarimu wa Vodacom ukiwafikia Kilwa Somanga, Kilwa Chumo na Ruangwa Namungo.