Zaidi ya familia 30 kutoka maeneo mbalimbali nchini Kenya walikusanyika mapema jana nje ya hospitali ya Malindi katika kaunti ya kilifi kwa ajili ya kupokea miili ya wapendwa wao iliyohifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti baada ya kufukuliwa msituni shakahola miezi kadha iliyopita.
Miili saba ilikabididhiwa kwa família tatu kwa ajili ya mazishi baada ya kupewa ushauri wa kisaikolojia na wanachama wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu.
Hii inajiri baada ya Mchakato wa uchungu wa utambuzi wa miili ambao umechukua mwaka, kwa sababu ya miili mingi ilikuwa imeharibika, uwepo wa idadi kubwa ya kesi, na ukosefu wa vifaa vya kufanya vipimo vyote vya vinasaba yaani DNA.
Katika ripoti iliyotolewa na tume ya kitaifa ya kutetea haki za binadaam ,wiki iliyopita iliwalaumu maofisa wa serikali kwa kuzembea kazinui na kushindwa kuzuia mauaji hayo.
Aidha familia za waathiriwa zimetoa wito kwa serikali kuzingatia ufadhili wa gharama za mazishi. Awamu ya tano ya kufukua miili zaidi katika msitu wa shakahola inatarajiwa kuanza tena baada ya miili iliyopo kukabidhiwa kwa familia.