Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili Wilayani Monduli Mkoani Arusha ameshiriki katia ibada ya kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Lengo kuu la ibada hiyo ni kuenzi na kukumbuka mchango mkubwa wa Hayati Sokoine katika maendeleo ya taifa.
Hayati Sokoine, aliyefahamika kama mzalendo wa kweli, alijitolea kwa dhati katika utumishi wake kwa wananchi na alikuwa na hofu ya Mungu katika kutekeleza majukumu yake.
Alizaliwa Agosti 01, 1934, kijijini Enguik, Monduli Juu wilayani Monduli, mkoani Arusha.
Tukio hili linatarajiwa kuwa fursa ya kuwakumbuka na kuenzi viongozi waliojitoa kwa dhati katika kuwatumikia wananchi na kuweka alama za kudumu katika historia ya taifa letu.