Baraza la Mitihani Tanzania NECTA limetangaza kuanza kwa Mitihani ya Kidato Cha Sita na Uwalimu nchi nzima ambapo mitihani hiyo itaanza siku ya kesho jumatatu tarehe 6 may 2024 na kumalizika tarehe 20 na 24 may mwaka huu na mtihani huu utafanyika katika jumla ya shule za secondary 931 na vituo 258 vya wanafunzi wa kujitegemea
Ratiba huyo imetangazwa Leo na Katibu Mtendaji wa NECTA, Said Mohammed wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam huku akisema kumekuwa na ongezeko la asilimia 6 la watahiniwa ukilinganisha na waliofanya mwaka jana 2023
Aidha ameongezea kuwa athari za mvua zimesababisha shule moja ya secondary ya kilwa huko Lindi kutokuweza kutumika na wanafunzi kufanyia mtihani wao katika kituo cha FDC (Chuo cha maendeleo ya jamii)