Justin Bieber na mkewe Hailey wameweka nyuma maisha yao ya zamani na kuganga yajayo hii ni baada tu ya wanandoa hao wakiwa wako tayari kumkaribisha mtoto wao wa kwanza.
Mnamo Mei 9, wapenzi hao walishiriki habari za furaha katika chapisho la pamoja kwenye Instagram kwamba wanatarajia mtoto wao wa kwanza wakiwa pamoja baada ya miaka sita ya ndoa.
Sasa, kulingana na Life & Style iliripoti kwamba Justin na Hailey wamekuwa wakishughulika na masuala ambayo si mazuri katika ndoa yao lakini, “wamefurahi sana kumkaribisha mtoto katika ulimwengu huu na wanaona maisha haya mapya kama nafasi ya kuweka nyuma matatizo na mapito yao ya nyuma na kuanza upya kama familia”
Mtu wa ndani aliwahikushiriki moja ya tukio la beiber na mkewe akisema, “Walifunga ndoa wakiwa wadogo sana na hawakuwa na mvutano wa kihisia na hata moyo kukabiliana nayo. Ilikuwa vigumu. Talaka ilionekana kuwa njia yao pekee ya kutengana kwao.”
Ripoti hiyo ilieleza kuwa Justin na Hailey “wametafuta ushauri wa mchungaji wao na kupata tiba inayowasaidia sana hadi sasa”
Chanzo hicho kilisema kwamba wanandoa hao mashuhuri wa Hollywood “wako mahali pazuri zaidi. Ndoa yao ni nzuri hivi sasa.”