Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema kuwa serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya husasani Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ambayo imekuwa ni msaada mkubwa katika kukabiliana na magonjwa ya moyo kwa watanzania.
Chalamila ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzunduzi wa Teknolojia ya kidigitali ya matibabu ya moyo ambapo ameeleza kuwa “Rais amejitahidi kutofautisha siasa na utaalamu katika sekta ya afya, taasisi ya Jakaya Kikwete imekuwa ni msaada mkubwa kwa watanzania katika matatizo ya moyo hivyo teknolojia hii itapunguza gharama na ulazima wa mgonjwa kuwa hospitali ili kupatiwa matibabu na badala yake anaweza kupata mwenendo wa matibabu hata akiwa mbali na hospitali.”