Kesi ya ugaidi inayomkabili Mchungaji Paul Mackenzie na washtakiwa wenzake 94 inaanza nchini Kenya leo Jumatatu Julai 8, 2024 huko Mombasa.
Hiki ni kipengele kimojawapo cha mauaji ya Shakahola. Mnamo Machi 2024, makaburi ya watu wengi yaligunduliwa katika msitu huu ulio karibu na Kilifi.
“Hii ni kesi muhimu kwani inahusisha mauaji ya watu wengi,” ndivyo Leah Juma, jaji kiongozi katika kesi hiyo, alivyoeleza ratiba ya wiki hii. Makumi ya mashahidi watasikilizwa hadi Alhamisi.
Hii ni mojawapo ya kesi muhimu zaidi ambazo mahakama ya Kenya imeshughulikia tangu uhuru wake. Katika mwaka mmoja, wachunguzi waligundua miili 429 katika msitu wa Shakahola na uchimbaji unaendelea.
Wahanga waliozikwa eneo hilo walikufa kwa njaa. Walikuwa waumini wa Kanisa la Kimataifa la Habari Njema, la Mchungaji Mackenzie ambaye alihubiri kufunga sana ili kukutana na Yesu. Kwa kuzingatia ukubwa wa kesi hiyo, mahakam ya Kenya iliamua kuigawanya katika kesi kadhaa, kuenea katika mahakama tatu tofauti.
Leo Jumatatu, kwa hivyo ni ile ya ugaidi ambayo inaanzia katika mahakama ya Shanzu mjini Mombasa. Paul Mackenzie na washirika wake 94 wanakabiliwa na mashtaka 13 yakiwemo itikadi kali, uhalifu na kuwezesha kitendo cha kigaidi.
Kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka, Paul Mackenzie na washtakiwa wenzake “walikubali na kukuza mfumo wa imani uliokithiri ili kuwezesha vitendo vya ukatili vinavyoendeshwa na itikadi.” Kwa hivyo kesi hii iko, kulingana na mwendesha mashtaka wa umma, chini ya sheria ya kupambana na ugaidi.
Jaji Leah Juma alieleza azma yake ya kusogeza mbele kesi hiyo bila kuchelewa. Siku nne za ziada za kusikilizwa tayari zimepangwa, kuanzia Julai 22 hadi 25.