Siku tano tu baada ya kunusurika kifo katika mkutano wa kampeni, Donald Trump alirejea jukwaani siku ya Alhamisi Julai 18. Alijifanya sio tu kama mtu aliyenusurika kifo kimiujiza bada ya kulengwa kwa risasi, lakini juu ya yote kama kiongozi mkuu asiye na shaka wa mrengo wa kulia nchini Marekani.
Donald Trump ameahidi “ushindi usio na kifani” kwa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba mwaka huu, akifunga kama nyota kongamano la chama lililokuwa likiendelea, huku wanachama wote wakiahidi kumuunga mkono katika kugombea kwake.
Nchini Marekani, maandamano haya ya umoja yalithibitishwa katika misa kuu iliyoandaliwa tangu Jumatatu Julai 15 huko Milwaukee, katika eneo la Maziwa Makuu. Inatofautiana na hali ya joto inayoongezeka kati ya Wanademocratic, ambao zaidi na zaidi wanamtaka rais anayemaliza muda wake Joe Biden kujiuzulu.
Siku tano baada ya kunusurika kifo katika tukio la risasi lililomjeruhi sikion, Donald Trump amerejea jukwaani, chini ya ulinzi mkali, akitoa hotuba iliyochukua takriban dakika 90 kama kiongozi mkuu asiyepingika wa mrengo wa kulia nchini Marekani.
Akiwa na bendeji inayoonekana wazi kwenye sikio lake la kulia, amekubali rasmi uteuzi wa Chama cha Republican, ambacho takriban wajumbe 2,400 walikuwa wamepiga kura zao siku ya Jumatatu.
“Kwa hivyo usiku wa leo, kwa imani na kujitolea, ninakubali kwa fahari uteuzi wenu kuwa rais wa Marekani ninagombea kuwa rais wa Marekani yote, sio nusu ya Marekani” , amesema katika hotuba yake. Lakini lafudhi yake ya kuunganisha hata hivyo ilibakia katika wachache ikilinganishwa na mada zake zinazogusia: uhalifu, uhamiaji, mfumuko wa bei.