Septemba 14, 2022 Kamati ya rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF ilitangaza kumpunguzia adhabu Msemaji wa Yanga Haji Manara kutoka milioni 20 ya faini aliyotakiwa kuilipa hadi milioni 10 huku hukumu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka miwili ikibaki palepale.
Sasa leo Septemba 15, 2022 Haji Manara amefunguka haya kupitia ukurasa wake wa instagram juu ya taarifa hiyo wakati alipokuwa Airport akimuaga binti yake Hamida ambae alikuwa akiekea nchini Uturuki kimasomo.