Marekani imetoa idhini kwa Ukraine kushambulia Urusi kwa makombora ya masafa marefu ambayo iliipa.
Afisa wa Marekani ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili, Novemba 17, akibainisha habari kutoka kwa vyombo vya habari vya Marekani.
Mabadiliko haya makubwa ya kimkakati yanakuja wiki chache kabla ya Donald Trump kuingia madarakani na saa chache baada ya shambulio kubwa la Moscow dhidi ya miundombinu ya Ukraine.
Silaha hizi zina upeo wa juu wa kilomita mia kadhaa zingeiwezesha Ukraine kufikia maeneo ya jeshi la Urusi na viwanja vya ndege ambavyo ndege zake za kivita huruka.
Lakini hadi sasa, kuhusu makombora ya ATACMS, Marekani ilikataa kutoa idhni hiyo, kwa upande mmoja kwa sababu Urusi ilionya kwamba ingechukulia hatua hiyo kama ongezeko kubwa la mashambulizi na kwa upande mwingine kwa sababu jeshi la Marekani liliamini kwamba wao wenyewe hawakuwa na makombora haya maarufu kwa wingi vile.