Utafiti uliofanywa na Wanasaikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Exeter, Uingereza umegundua uhusiano uliopo baina ya elimu na magonjwa ya akili ikisemwa kuwa watu waliofika hatua ya Chuo Kikuu wana asilimia ndogo ya kupata magonjwa ya akili ukilinganisha na watu ambao hawakufikia kiwango hicho.
Utafiti huu ulihusisha watu zaidi ya 2,315 wenye umri wa miaka 65 ambapo zaidi ya nusu ambao hawakufika elimu ya Chuo Kikuu walionesha dalili za magonjwa ya akili kama Dementia na Alzheimer huku waliofika hatua hiyo wakionesha kutokuwa na dalili ya magonjwa hayo.
Profesa Linda Clare, Mtaalamu wa mambo ya ubongo alisema:>>> “Mara nyingi watu wanaopata magonjwa ya akili wanapofikisha umri mkubwa ni watu ambao hawakupata elimu kubwa. Hii ni kwa sababu kupata elimu kunakusaidia kushughulisha akili. Hivyo ni vigumu kupatwa na magonjwa yanayoathiri ubongo.”
VIDEO: Ulipitwa na hii ya Mrema kumwambia Mbatia atimize ahadi yake la sivyo atavua nguo?Ukitaka kujua ni ahadi gani, bonyeza play video hapo chini…
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo