Kanye West anakabiliwa na shtaka jingine la utovu wa nidhamu, safari hii kutoka kwa mwanamitindo aliyemtuhumu kwa unyanyasaji wa kijinsia wakati wakifanya video ya wimbo wake mwaka 2010 akiwa video vixen.
Mwanamke huyo, mshiriki wa zamani wa America’s Next Top Model Jenn An, aliwasilisha kesi hiyo huko New York mnamo Ijumaa (Novemba 22), kwa The Wrap.
Anadai kuwa mnamo Septemba, 2010 alikuwa kwenye seti ya video ya La Roux ya “In for the Kill,” wimbo ambao West anaonekana kwenye remix.
Anadai kuwa West alimchagua kuwa kwenye video kwa kusema, “Nipe msichana wa Kiasia.”ambapo alianza kumshika na kumnyonga kwa makusudi akinekana kufurahia tukio hilo taarifa iliyoripotiwa na shirika habari la NBC
Mlalamikaji wa tuhuma hizo ambaye aliyekuwa mcheza video (video vixen) anadai fidia na hatua kali kuchukuliwa dhidi ya Ye.