Kijana aliyejirekodi akiendesha gari kwa magoti kabla ya kusababisha ajali iliyo pelekea mwanamke aliyemgonga kupooza kutoka shingoni kwenda chini amefungwa jela kwa miaka miwili na miezi miwili.
George Taylor, 19, wa Stretham, Cambridgeshire, alirekodi video tano akiendesha Volkswagen Golf kwa kasi na magoti yake kwenye usukani alizua mtafaruku mkubwa kwa familia na marafiki wa mama huyo.
Polisi wa Norfolk walisema alikuwa na leseni yake kwa chini ya wiki 12 tarehe 18 Januari mwaka jana, na alipiga simu mbili na kutuma ujumbe wa maandishi wakati akiendesha gari.
Karibu saa 11 asubuhi, aligonga gari kwa nyuma iliyokuwa ikingoja kugeuka kulia mbele yake huko A47 huko East Tuddenham, na hii ilitokea baada ya kushindwa kuiona.
Ndipo mwanamke anayeitwa Catherine mwenye umri wa miaka 40 wakati huo akiachwa akiwa amepooza kutokana na mshtuko na mgongano huo.
Kwamujibu wa SKY News inasemekana Mama sasa anahitaji utunzaji wa maisha yote kwani amepooza.