Mwanasheria wa Mchezaji Feisal Salum amesema hajui chochote kama Mchezaji huyo atarejea Yanga au la na kwamba hana chochote cha kuwaambia Mashabiki wa Yanga.
Alipoulizwa kuhusu ‘status’ ya Feisal na ni Mchezaji wa Timu gani kwa sasa, Mwanasheria huyo amesema “bado, siwezi kuongea lolote”
Mwanasheria huyo pia alisema hawezi kusema lolote kuhusu kilichompeleka Feisal Dubai na kwamba kwa sasa Mchezaji huyu atakuwa akipatikana Zanzibar.