Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imesema kwa kipindi cha mwaka mmoja ofisi yake imepokea kesi zaidi ya 500 za malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi dhidi ya Serikali.
Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Neema Ringo wakati wa uzinduzi wa kamati ya ushauri wa kisheria uliofanyika Jijini Mwanza, ambapo amesema wamepokea idadi hiyo ya kesi za wananchi kuishtaki Serikali, hivyo kuundwa kwa kamati ya ushauri wa kisheria itasaidia kupunguza kesi hizo.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amewaagiza wakuu wa wilaya kuunda kamati za ushauri wa kisheria kama ilivyoagizwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ili kusaidia kupunguza migogoro na kufanikisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.