Wanandoa wa Uingereza waliozuiliwa nchini Iran kwa shutuma za kuipeleleza nchi hiyo wameshtakiwa kwa ujasusi, kwa mujibu wa shirika la habari la mahakama la Iran.
Bw na Bi Foreman walikamatwa mwezi Januari lakini habari za kuzuiliwa kwao, kwa tuhuma za usalama ambazo hazijatajwa, zizoibuka wiki iliyopita.
Msemaji wa mahakama alisema kwamba wanandoa hao, wote wenye umri wa miaka 52, “waliingia Iran kwa kisingizio cha watalii” na “kukusanya habari katika mikoa mingi ya nchi”.
Wanandoa hao walihama kutoka East Sussex na kuanza maisha mapya huko Andalucia, Uhispania, mnamo 2019 na walikuwa wamejitokeza kwenye kipindi cha Channel 4’s A New Life in the Sun mnamo 2022 ili kuonyesha maisha yao kama wahamiaji.
Wanandoa hao, wote wenye umri wa miaka 52, walikuwa wamesafiri kwa pikipiki kote ulimwenguni na walikuwa wamepanga kukaa Iran kwa siku tano.