Jumatatu ya June 26, 2017 zipo habari kubwa ambazo zimepewa kipaumbele kwenye mitandao mbalimbali na Radio na Televisheni na nyingi kati ya hizo ni zile zinaingia moja kwa moja katika maisha ya siasa, utamaduni, uchumi na jamii.
Kama zilikupita nimekukusanyia mambo yote makubwa ambayo yamepewa uzito siku ya leo na imekusogezea hapa na unaweza kuyapata kuitia millardayo.com
"Umekaa uwaziri mkuu miaka 10 halafu unakuja kusema nchi imepoteza dira, ningekuwa mimi ndiye Rais ningemuweka ndani"-Lubinga #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Spika Ndugai juzi aliwadokezea wabunge kuwa kuna uwezekano wa kuongezwa muda wa bunge hilo kwa ajili ya mambo muhimu #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
TFDA yazuia kuuzwa unga wa sembe kutoka kampuni ya Family Super baada ya kubainika inakiuka utaratibu kwa kuuza kabla ya kukaguliwa #UHURU
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Mkoa wa Kilimanjaro umetajwa kuwa ndio mkoa unaoongoza nchini kwa uzalishaji wa mihadarati ukifuatiwa na mkoa wa Arusha #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Imeelezwa kuwa TAKUKURU sasa inachunguza mkataba wa kampuni ya kimataifa ya kuhudumia shehena ya kontena bandarini 'TICTS' na TPA #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Serikali imeamuru ukaguzi wa kifedha na kufuatilia vituo vya watoto yatima ili kujiridhisha kama kuna uwazi wa matumizi ya fedha #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Serikali kupiga marufuku uagizaji wa chaki kutoka nje ya nchi kufuatia upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Familia ya marehemu Salum Mohammed, aliyeuawa na polisi siku 43 zilizopita inatarajia kumzika June 30 mwaka huu #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Lowassa amemtaka JPM kuwaachia huru Masheikh wa uhamsho wanaoshikiliwa kwa zaidi ya miaka minne kutokana na tuhuma za ugaidi #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Baadhi ya WaTZ wapo hatarini kupofuka macho kutokana na vitendo vya kununua miwani mitaani na kuivaa kama urembo bila kupimwa #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Watu 24 kati ya 100 wamebainika kuacha kutumia ARV's sababu ya umbali mrefu wa vituo na kupuuzia baada ya kupata nafuu #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Serikali imekamata shehena ya mahindi zaidi ya magunia 1,639 Kilimanjaro yakitoroshwa kwa njia ya magendo kwenda Kenya na Ethiopia #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Imeelezwa futari zilitumika kwa mikakati tofauti baadhi ya wanasiasa waliitumia kuongeza ushawishi wao, wengine kusisitiza amani #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Waziri Mwigulu Nchemba ametishia kufuta usajili wa NGOs zitakazoendelea kudai haki ya watoto wanaopata mimba kurejeshwa shule #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Imegundulika kuna shehena kubwa ya mahindi imekuwa ikisafirishwa nje kila siku kutoka wilaya za Rombo na Moshi mkoani Kilimanjaro #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 26, 2017
Baada ya JPM, Waziri Nchemba naye ametoa marufuku!!!