Toka nimeanza kuandika na kufatilia habari sijawahi kusikia jeshi la nchi limechukua hatamu kuendesha mashindano ya urembo tena mashindano yanayokutanisha warembo kutoka sehemu mbalimbali za taifa ili kumtafuta mshindi.
Stori hii ya kipekee inatokea Uganda ambapo jeshi la nchi hiyo limeamua hivyo baada ya kuona ubabaishaji unaofanywa na Waandaaji wa Miss Uganda shindano ambalo halikufanyika kwa miaka kadhaa kutokana na ubabaishaji.
Ripota wa TZA Kampala Bill the African, ameripoti kwamba mmoja kati ya wenye vyeo vyao jeshini ambae pia ni mdogo wake Rais Museven amesema jeshi limeamua kuchukua usimamizi wa mashindano haya kwa madai kwamba ni njia ya kuwavutia vijana wapende kilimo kitakachotangazwa kupitia haya mashindano ikiwa tayari pia jeshi hilo limechukua Wizara ya kilimo kwa ajili ya kuiongoza.
Bill alipozunguka mtaani kuwauliza watu maoni yao imekua 30 kwa 70 yani kuna ambao wanaona hakuna shida Wagumu hawa kuongoza mashindano hayo lakini wengine wengi wanapinga wakisema Jeshi hili linajulikana kabisa huwa halicheki na mtu wala halina urafiki na Raia sasa ndio wataweza kuendesha mashindano ya Urembo? ni vitu viwili tofauti kabisa.
Kabla hujaondoka hapa ningependa uniachie maoni yako, ni sahihi kwa kilichofanywa na jeshi?
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB