1. Wengine wananikejeli wanasema kwa shughuli hii ya bunge la katiba naonyesha sifai Urais, mimi sijaomba Urais…. naifanya kazi hii kama Mwenyekiti wa bunge la katiba… basi, lakini nasema wanaochagua ni Wananchi… inawezekana mwakani wakatamani mtu mzima alietulia, asieogopa Wapuuzi, mtu makini, mwadilifu… kama itakua hivyo wajue tu kuna sisi wengine wa kuweza kufikiriwa kwa mambo kama hayo.
2. Wananchi wengi wameonyesha shauku ya kuja kwetu hapa kinyume na ambavyo imekua ikitangazwa, makundi mbalimbali ya Wananchi yaliyosoma rasimu yamebaini kwamba rasimu ina mapungufu kama ambavyo sisi ndani ya kamati tumeona ina mapungufu, hili sio jambo la ajabu wala sio kupuuza kazi iliyofanywa na tume, hapana…. tume ilifanya kazi yake vizuri.
3. Tukumbuke kwamba Tume ilipokea maoni kwa Wananchi zaidi ya laki 3 na mabaraza 700, walichokileta ni tafsiri yao kuhusu maoni yao…. mnielewe vizuri hapo, na wao walikaa wakachambuuaaaaa, mengine wakayachukua, mengine wakayakataa, mengine wakayarekebisha.
4. Katiba tunayoitunga iwe ni katiba ambayo itawezesha sheria zitakazokua rafiki kwa Watanzania wote,
5. Nawasihi ndugu Wajumbe msifadhaike na maneno ya kejeli watu wanazungumzia posho na vitu vingine, mimi mwenyekiti wenu niko imara kabisa na kwa hulka yangu mimi hizi kejeli na matusi ni kama vile maji kwenye mgongo wa bata, halowani…….. wengine tunaanza kuwabaini, kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Kubenea.
6. Kuna Mfadhili na Wafadhili nyuma yake wanamsogeza mbele kwa sababu wameona vipaji vyake kwa hiyo tuwaone nao……………. kuna njia nyingi za kupata riziki tuwasamehe tu.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB