Shule ya Msingi Namlonga iliyopo Kijiji cha Namlonga Kata ya Manyara takribani kiliomita 45 kutoka Makao Makuu ya Mkoa wa Songwe matokeo ya darasa la saba msimu wa 2018 ilishika nafasi ya mwisho Kimkoa kati ya shule 420 na nafasi ya mwisho kiwilaya kati ya shule 161.
Mkuu wa shule hiyo Hassani Mlilo amesema walipewa bendera hiyo waipeperushe na viongozi wa Halmashauri ya Mbozi kama fundisho kwa walimu na viongozi wa kijiji na kata kutokana na matokeo hayo mabaya ambayo hayajawahi ikumba shule hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1991.