October 28 2014 saa nane mchana kilionekana kifaa kwenye takataka ambapo iliaminika ni bomu hivyo Polisi wakapewa taarifa na kuwasili kwenye eneo la tukio saa kumi na moja jioni, wakakagua na kuomba ndoo mbili za mchanga wakalikagua kwa nusu saa alafu wengine wakabaki baada ya baadhi yao kuondoka.
Kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda, saa moja na dakika 45 usiku Wanajeshi walifika kwenye eneo hilo na kulikagua na kusema lile halikua bomu la kawaida, ni kombora ambalo lilitegwa miezi miwili iliyopita na lilikua tayari kulipuliwa ambapo kama lingelipuka lingeweza kuathiri eneo kubwa sababu ya nguvu yake kubwa.
Eneo lilikokutwa bomu hili ni Kijitonyama Dar es salaam karibu na kanisa la KKKT ambapo wakati huu tunasubiria maelezo ya Polisi, tumeyakusanya hayo yote hapo juu ambayo yametolewa na mashuhuda.