Rubani Irene Koki Mutungi alizaliwa 1976 na wazazi wake wote wakiwa wakenya, baba yake mzazi aliwahi kuwa rubani mwenye leseni ya kuendesha ndege za biashara akifanya kazi Kenya Airways wakati huo, Koki alisoma Moi Girls Nairobi na baadae alipomaliza elimu ya juu 1992 akiwa na miaka 17 alianza kujifunza mafunzo ya kuendesha ndege.
Koki alianza kujifunza mambo ya ndege katika shule ya Wilson Airport nchini Nairobi ambapo alihitimu na kupata leseni ya kuendesha ndege binafsi lakini aliendelea tena na mafunzo ya ndege Oklahoma City nchini Marekani na baadae kufanikiwa kupata leseni ya kuendesha ndege za biashara (abiria) na mamlaka ya anga Marekani FAA.
Irene Koki Mutungi alirejea Kenya mwaka 1995 akitokea Marekani na kupata ajira katika shirika la ndege la Kenya (Kenya Airways) ambapo alifanya kazi kama mwanamke wa kwanza rubani katika taifa hilo, rekodi ambayom alidumu nayo kwa miaka sita baada ya Kenya kupata rubani mwingine mwanamke.
Mwaka 2004 Irene alifanikiwa kupata leseni ya kuendesha ndege kubwa za abiria na kuweka rekodi ya kuwa rubani wa kwanza wa kike Afrika kupata leseni ya kuendesha (Commercial aircraft), baada ya kufanikiwa kuendesha ndege aina ya Boeing 737, baadae hii Boeing 767 na baadae ndio akafuzu kuendesha Dreamliner Boeing 787, waajiri wake April 15 2014 walimtangaza kama mwanamke wa kwanza kuwahi kuendesha Dreamliner Africa.
EXCLUSIVE: Kutana na kijana mwenye miaka 22 anayetengeneza Robot