Moja kati ya habari kubwa kwa upande wa soka leo nchini Tanzania ni pamoja na Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC kukubali kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Nkana FC ya Zambia katika game ya round ya kwanza ya CAF Champions League ilyochezwa mjini Kitwe Zambia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo wa Azam TV Zakazakazi, Simba SC imekuwa haina historia nzuri dhidi ya Nkana, hivyo kupoteza leo haikuwa mara ya kwanza kupoteza mchezo dhidi ya Nkana, naambiwa Simba leo imepoteza kwa mara ya tatu dhidi ya Nkana toka ipoteza mara mbili tofauti na kutolewa mwaka 1994 robo fainali na mara ya pili 2002 hatua ya mtoano kama hii.
Nkana walifanikiwa kuvuna magoli kupitia kwa Ronald Kampamba dakika ya 27 na Kelvin kampamba dakika ya 56 wakati nahodha wa Simba John Bocco ndio alifunga goli la kufutia machozi la Simba dakika ya 73 kwa mkwaju wa penati, Simba sasa itahitaji ushindi wa kuanzia goli 1-0 katika mchezo wa marudiano ili iitoe Nkana kwa mara ya kwanza katika mchezo utakaochezwa uwanja wa Taifa.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe