Watu saba waliohusika katika mashambulizi tofauti ya kibaguzi dhidi ya fowadi wa Real Madrid Vinicius Jr wameadhibiwa na Tume ya Taifa ya Uhispania dhidi ya Ukatili, Ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na kutovumiliana katika Michezo, Tume ya Michezo ya nchi hiyo ilisema Jumatatu.
Wanaume wanne walitozwa faini ya Euro 60,000 (£51,700) sawa na zaidi ya tsh millioni 152,na kufungiwa kumbi za michezo kwa miaka miwili baada ya kuning’iniza bango lenye maandishi “Madrid hates Real” na sanamu nyeusi yenye mvuto katika mfano wa shati nambari 20 ya Vinicius kwenye daraja karibu na majengo ya Real kabla ya mechi ya Kombe la timu dhidi ya Atletico Madrid Januari 26.
Watu wengine watatu walitozwa faini ya €5,000 (£4,300) sawa na tsh million 12,671,276 na kufungiwa kumbi za michezo kwa mwaka mmoja baada ya kutoa ishara za kibaguzi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil wakati wa mechi ya LaLiga kwenye Uwanja wa Mestalla huko Valencia mnamo Mei 21.
hayo yamekuja siku 11 baada ya kukamatwa kwa watu hao wanne kwa tuhuma za kutundika sanamu hiyo na kuachiliwa kwa dhamana na mahakama ya Madrid.
Vinicius Jr amekuwa akigonnga vicha mbalimbali vya habari za michezo baada ya wiki kadhaa zilizopita kuziita LaLiga na Uhispania kuwa za ubaguzi wa rangi kufuatia dhuluma alizopata wakati wa mechi ya Real dhidi ya Valencia.