Tanzania inaomboleza kifo cha rapper Geez Mabovu ambae amefariki kwao Iringa akiwa hospitali jioni ya November 12 2014 baada ya kuugua kwa kipindi kirefu, ni wiki mbili toka aondoke Dar es salaam akiwa na hali mbaya kiafya.
Baada ya kifo chake kumekua na maneno au taarifa nyingi zinazoandikwa kwenye mitandao mbalimbali ambapo baada ya Roma Mkatoliki kukutana nazo ameamua kuandika yake ya moyoni kama ifuatavyo.
>>> Lawama zinakuwa nyingi sana naona!!! na wengi mnazipeleka eneo moja tu!! Askwambie mtu hakuna watu wenye #Stress kama sisi #wasanii aaaf mbaya zaidi sisi wengi wetu hatuwezi kuishinda hiyo #Challenge finally tunafail!! Kuna kipindi msanii unakuwa #Juu sana na hiyo inatokana na juhudi zako na support unayopewa na wadau wa mziki (media sanasana) na mashabiki!! #HALAFU GHAFLA FROM NOWHERE ULE UJUU UNAANZA KUPUNGUA KISHA UNAISHA KABISA!! AU KUNA WAKATI HUO UJUU HAUISHI TARATIBU UNAISHA GHAFLA TU VUUUP!! #STRESS INAANZA!! SWALI NI KWANINI HUO UJUU UNAISHA GHAFLA!!?
>>> ‘Je uwezo wako unaisha? Unaridhika mafanikio? Unaikosa ile support ya awali toka kwa wadau? Je unashushwa kwa nguvu za watu fulani? Kuna wengine sasa wasanii wanakuwa hawajawahi kuwa #JUU Lakini wanafight kufika juu na wanajituma hasa na #NI_WAKALI sana lakini zinatokea tu #FIGISUFIGISU msanii anakuwa hatoboi!! Finally anaamini anabaniwa na hapewi support. ..#STRESS INAANZA!! Wasanii kama #GEEZMABOV tunao wengi sana hapa #TANZANIA lakini hatujifunzi kwa mifano!!’
>>> ‘Kuna vipaji havipaswi kupuuziwa hata kidogo jamani vipeni support a hundred please!! Hatatokea msanii kama #AfandeSelle mi nakwambia hadi leo ni mkali sana huyu mtu!! Hakuna #Rapper kama #JosMtambo askwambie mtu!! Yule #Enika yule ni anaimba jamani acha tu!! Hawa vijana wa #TamaduniMusic ni new #faces zinazokuja vizuri sana wapewe #support!! #Joslin#MBDog# hawa watu ni #Almasi jamani!! Tunawasanii wakali kibao mi nakwambia‘
‘DojoNaKaya ni #nyoko!! Wataimba wote ila mtu kama #RamaDee ni hadithi nyingine ujue!!! Na isiwepo hii hali ya kwamba “ILI ATOBOE FLANI BASI LAZIMA FLANI APOTEE!! HII KAULI HAINA MASHIKO KIUKWELI!!! Kwanini apotee?? Si tuwe wote tu!!! Na msitetee kwa kusema HATA MAREKANI IKO IVO…kwani si wao!! Ni lazima tuwaige kwani!!?
Roma akaandika tena kwenye post nyingine Instagram >>> ‘ILA UPANDE WA PILI SASA Lakini wakati mwingine sisi wasanii tuna makosa kutokana na #ATTITUDE zetu…tutambue kuwa tunaofanya nao kazi ni #WAFANYABIASHARA na sio ndugu zetu wala hakuna sehemu iliyoandikwa NI LAZIMA WAKUSUPPORT!! Kila mtu ana matakwa yake kama mfanyabiashara kama mdau!! So #JIONGEZE!!
‘Tuna #Angle moja tu sasa ya biashara ya muziki wetu nayo ni #SHOW Sasa kuna wasanii unapita #Mwaka hawajapata show na ni wakali sana…na mbaya zaidi bado hawapati #AIRTYM katika media houses!!#WANAUMIA SANA!!!!! Kama hiyo haitoshi msanii ana miezi 6 hajapata show wala akiaandaa mwenyewe mashabiki hawamsupport anafail…kisha anaskia msanii mchanga tu ametoka juzi amepigiwa simu ya show #MILIONI3 Amekataa!! Wakati yeye anaitafta hata show ya #LAKI3 tu hapati!!’
‘STRESS INAANZA!! Finally ukishindwa kui control stress basi uta end up into NEGATIVE SIDE!!! Wito wangu tafadhali tuwasapoti na tuzidi kuwasapoti vijana wetu wenye vipaji…najua wapo wenye matatizo lakini tusiikate tamaa tuzidi kuwaonyesha njia bora ya mafanikio…hii ni kwenu mashabiki na wadau wa muziki wetu huu pendwa wa BONGOFLAVA’