Kazi ya Millard Ayo ni kukusanya na kukusogezea habari zote kubwa na breaking news zote za michezo, siasa, uchumi, burudani na jamii kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na mchana wa leo June 29, 2017 nimekukusanyia hizi story 10 zilizopewa uzito mkubwa.
Miongoni mwa story kubwa ni pamoja na Rais Trump kuongeza masharti mapya ya maombi ya Visa kwa mataifa 6 ya Kiislamu na wakimbizi akisema lazima uwe na mtu anayeshirikiana na Marekani.
Rais wa TFF Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa, Rais wa Simba Aveva na Makamu wake Kaburu wamefikishwa mahakamani Kisutu muda huu. pic.twitter.com/LLwezf3X2G
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
BREAKING:Rais wa Simba Aveva na makamu wake Kaburu wametuhumiwa kwa makosa matano ambayo hayana dhamana, kesi yao itasikilizwa July 13 2017. pic.twitter.com/EPvrAWN43C
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
TANESCO watafanya marekebisho ya kituo cha kupooza Umeme eneo la Kunduchi July 2,2017, kuna maeneo yatakayokosa umeme saa 2 hadi 9 Alasiri. pic.twitter.com/8g6BcMGZT5
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Polisi nchini Australia imemshitaki Kadinali wa kanisa Katoliki mwenye ushawishi mkubwa George Pell kwa makosa ya kunyanyasa watoto kingono. pic.twitter.com/GUmlTqdCDd
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Rais Magufuli amemtumia salamu za pole Rais wa AfDB kufatia kifo cha Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Afrika/Afrika Kusini Dr Tonia Kandiero pic.twitter.com/6kUM14GwmR
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Watumishi wanaofanya kazi serikalini nchini Kenya wataanza kulipwa nyongeza ya mshahara kati ya 5.2% hadi 30.7% kuanzia July 1, 2017. #RFI pic.twitter.com/e0xzOpTXLa
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Uchunguzi wa Benki Kuu ya Kenya umeonesha mawakala wa miamala ya fedha kwenye simu walikuwa na kesi 24,562 za pesa bandia ambayo ni sawa 97% pic.twitter.com/iIkHoa4R4N
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Rais Trump ameongeza masharti mapya ya maombi ya Visa kwa mataifa 6 ya Kiislamu na wakimbizi, lazima uwe na mtu anayeshirikiana na Marekani. pic.twitter.com/5GyQmsxdvo
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
Vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini COSATU vimeitaka serikali kufanya mkutano wa kubuni mipango endelevu ya kutatua tatizo la ajira. pic.twitter.com/zC4KyEZYaa
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
BURUNDI: Rais Pierre Nkurunziza amezindua maadhimisho ya miaka 10 tangu Burundi ijiunge na EAC, ameahidi nchi yake haitajitenga na umoja huo pic.twitter.com/rxRe7K9D16
— millardayo (@millardayo) June 29, 2017
EXCLUSIVE: Benjamin Wa Mambo Jambo amerudi…alikuwa wapi na anafanya nini? Majibu anayo kwenye VIDEO hii!!!