Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO Watu 77 hufariki dunia kila siku Tanzania kutokana na ugonjwa wa kifua Kikuu huku mkoa wa Dar-es-salaam ukitajwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaougua ugonjwa huo kwa asilimia 20.
Akizungumza na Waandishi wa habari Dodoma leo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kutokana na hali hiyo zaidi ya shilingi milioni 35 zinatumika kugharamia matibabu ya mgonjwa wa kifua kikuu sugu.
Waziri Ummy Amewasisitiza wananchi kuwa TB inatibika na dawa zake zinatolewa bure katika vituo vya umma na binafsi nchini na kueleza jitihada zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo ikiwemo kuimarisha mfumo wa uchunguzi na ugunduzi wa TB.
NACTE yazungumza kuhusu mfumo wake mpya wa kuhakiki Udahili