Moja ya story ambayo leo July 21, 2017 imekuwa ikimake headlines kwenye mitandao mbalimbali ni kuhusu mwimbaji staa wa Bongofleva, Baraka The Prince kuachana na label ya Rockstar4000 aliyosaini kufanya nayo kazi 2016.
Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Baraka ambaye amefunguka>>>”Wamecheza part yao kwa uwezo wao vizuri kabisa. Kuna vitu sawa wamenifanyia ndio na wapo kwenye historia yangu na sitowasahau kwa jitihada zao walizonionesha. Sijaondoka kwa nia mbaya.
“Album yangu na kila kitu changu kuanzia leo kitakuwa chini ya label ya Bana Music na sipo chini ya mtu yeyote. Naomba kusema mashabiki wafahamu hii ni biashara na sio wanaanza kuongea vibaya.” – Baraka The Prince.
Beka wa Yamoto Band ashikiliwa na Polisi toka saa 5 asubuhi!!!!!