Nafahamu hii inaweza kukushtua sana, imetokea nchini Afrika Kusini kumuhusu mchungaji Lethebo Rabalago wa Kanisa la Mountzion General Assembly lililopo mji wa Limpopo, ambaye amekutwa akiwapulizia dawa ya kuua wadudu kwa madai kwamba itawaponya matatizo yao.
Mchungaji wa Limpopo Afrika Kusini awa gumzo, ni baada ya picha kusambaa akiombea watu kwa kuwapulizia dawa ya Mbu kanisani kwake Mount Zion pic.twitter.com/P6jOOAjmoh
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
Mchungaji aliyezua gumzo kwa kuwaombea watu kwa kuwapulizia dawa ya Mbu South Africa aliwahi kusema chochote kinafaa kwa uponyaji akitamka. pic.twitter.com/b2VAbzx30t
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
Kupitia picha alizozishare kwenye ukurasa wake wa Facebook, ameonekana akiwapulizia dawa hizo waumini kwenye sehemu mbalimbali za mwili na kueleza kwamba yeye kwake kila kitu anaweza kukifanya kuwa baraka za uponyaji.
Sasa muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa na picha za Mchungaji huyo akitumia dawa ya kuua wadudu kuwapulizia waumini kanisani kwake, Kampuni inayotengeneza dawa hizo iitwayo Doom imetoa tamko lake na kumuonya mchungaji huyo kuacha mara moja kutumia bidhaa zake kwa matumizi ya aina hiyo.
'Stop spraying our product in people's faces,' Tiger Brands tells #DoomPastor https://t.co/Pk9vr8KOMu #BBCAfricaLive #SouthAfrica pic.twitter.com/xDFBh2jbpL
— BBC News Africa (@BBCAfrica) November 21, 2016
Na tayari imetoka taarifa kuwa vyombo vya usalama nchini Afrika Kusini vimeanza uchunguzi juu ya tukio hilo la mchungaji.
South African 'Pastor of Doom' investigated https://t.co/wwdHSqU73A
— BBC News Africa (@BBCAfrica) November 21, 2016
Nimekuwekea picha hapa chini.
VIDEO: Ilikupita hii ya vurugu za Arusha zilizoibuka kanisani baada ya bwana harusi kudaiwa kuoa wakati ana mke mwingine? Itazame hapa