Baada ya Rais John Magufuli kutangaza kutoa vitambulisho 670,000 kwa Machinga, mchakato huo umeanza kutekelezwa katika baadhi ya maeneo ikiwemo soko la Mwenge jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia mchakato huo, Katibu Tawala wa Kinondoni, Stella Msofe amesema wafanyabishara wamejitokeza kwa wingi na wamejikita eneo hilo wakiamini ni sehemu ambayo itarahisisha kuwapata Machinga kwa urahisi.
Msofe amesema malengo yao ni kupata Wamachinga 5000 ambapo hadi sasa wameshatoa vitambulisho kwa Machinga 315 huku idadi kubwa wapo katika Data Base hivyo wanawafahamu.
“Ushauri ni kwamba Machinga wajitokeze na wawe halali, kwani lengo ni kuwafanya wafanye kazi katika mazingira salama,”amesema.