Chama cha ACT Wazalendo kupita kwa Katibu wa Uenezi wa Chama hicho Ado Shaibu kimeitaka Serikali na Bodi ya Korosho Tanzania kuharakisha usambazaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo Sulphur zenye ubora kwa wakulima wa Korosho.
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu amesema Serikali na Bodi ya Korosho zimeshindwa kujibu hoja walizozitoa kuwa ilitangazwa pembejeo za korosho zitagawiwa bure kwa wakulima lakini hadi sasa bado kuna uhaba.
>>>”Bodi imekwepa hoja ya msingi tuliyoitoa. Hakuna aliyesema wakulima wamezuiwa kununua pembejeo, tunachosema kutotoa taarifa sahihi na elimu kwa wakulima na wafanyabiashara, imesababisha uhaba wa Sulphur.” – Ado Shaibu.
July 30, 2017 ACT Wazalendo kilitoa matokeo ya utafiti wake juu ya usimamizi mbovu wa zoezi la usambazaji wa pembejeo za Korosho hasa Sulphur kwenye mikoa inayozalisha ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga ambayo huzalisha zao hilo kwa wingi wakisema licha ya nia njema ya zoezi la kugawa pembejeo bure mchakato huo umeleta usumbufu na kadhia kwenye sekta ndogo ya korosho na kutishia ustawi wa zao hilo.
Aidha, August 2, 2017 Maafisa Waandamizi wa Bodi ya Korosho, Mwanasheria na Katibu wa Bodi ya Korosho walitolea ufafanuzi suala hilo.
ULIPITWA? Madai ya ACT Wazalendo kuhusu kuhujumiwa kwa zao la Korosho…play kwenye video hii kutazama!!!