Miongoni mwa issue kadhaa zilizojadiliwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo July 24, 2017 ni pamoja na issue ya mkazi mmoja wa Ubungo Kibangu Dar es Salaam Adrian Mpande kunusurika kifo baada ya kupigwa risasi wakati akiingia Kanisani.
Tayari millardayo.com imezikusanya na kukuwekea pamoja issue zote kubwa kutoka katika Magazeti ya Tanzania leo July 24, 2017 ambazo hukuwekea kwenye twitter ya @millardayo.
Mkazi mmoja wa Ubungo Kibangu, Dar es Salaam Adrian Mpande amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi wakati anaingia Kanisani. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Imeelezwa kuwa sababu ya baadhi ya mikoa kuwa na hali mbaya ya Watumishi ni wafanyakazi kukimbia kufanyiwa vitendo vya kishirikina. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
DC Temeke amewataka Askari wastaafu wa Jeshi la Magereza kuepuka kujihusisha na vitendo vya uhalifu baada ya kuanza maisha mapya. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
CHADEMA Kanda ya Kati imelaani kukamatwa ovyo viongozi wao wa juu na kuwekwa mahabusu kwa muda mrefu bila kupelekwa Mahakamni. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Hatma ya Tundu Lissu kufikishwa Mahakani au la, itajulikana leo baada ya kushikiliwa na Polisi kwa siku 5 kwa tuhuma za uchochezi #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Rais Magufuli amewakosoa baadhi ya watendaji wa Serikali waliombeza Mbunge wa zamani David Kafulila wakati wa sakata la Escrow. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Mbunge Haonga (CHADEMA) ameitwa kuhojiwa na RPC Songwe baada ya bendera za chama hicho kupepea kwa wingi ktk Mji wa Mlowo, Mbozi. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Wanafunzi 16 wa Sekondari, 7 kati yao wa shule moja ktk H'shauri ya Wilaya ya Morogoro, wamekatisha masomo baada ya kupata mimba. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Tanzania imeanza majaribio kudhibiti sumu kavu ktk mazao kwa kutumia bidhaa ya kibaiolojia ya Aflasafe iliyotengenezwa na IITA. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
TAKUKURU mkoani Mara imewafikisha Mahakamani maofisa wengine watatu wa Idara ya Uhamiaji wakidaiwa kuomba na kupokea rushwa. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Wakazi watatu wa Igunga, Tabora wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na Dawa za Kulevya aina ya Heroin. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
M/kiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili, Prof. Lipumba ametakiwa kuondoka kwa hiyari kabla ya kuchukuliwa hatua nyingine. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Wakulima na wauza mwani Z'bar wamelalamika kodi kubwa wanazotozwa ktk ngazi mbalimbali wakati bei ya zao hilo ikiwa ndogo. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
CHADEMA wilayani Chemba, Dodoma inajipanga kumfungulia kesi DC Odunga baada ya kumsimaisha M/kiti wa kijiji bila sababu. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Wizara ya Afya Visiwani Zanzibar imepiga marufuku matumizi ya sigara katika maeneo ya wazi na sehemu za kutolea huduma za umma. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
TAKUKURU imeagizwa kuwakamata, kuwahoji Kaimu Mkurugenzi wa H'shauri ya Mbozi na Wakuu watatu wa Idara kwa matumizi mabaya ya fedha. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewaonya wanasiasa wanaotoa kauli za uchochezi, kumkejelei JPM kuwa watachukuliwa hatua. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Wabunge wa Upinzani wameshauriwa kujifunza kupitia kwa Mbunge @zittokabwe kushirikiana na Serikali ktk kuwaletea maendeleo wananchi. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
Rais Magufuli amepongeza kitendo cha aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) David Kafulila kuibua kashfa Tegeta Escrow. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 24, 2017
ULIPITWA? Kitu Zitto Kabwe ameongea mbele ya Rais Magufuli Kigoma…bonyeza play kwenye hii video!!!
VIDEO: “Usipofanya kazi hautokula na usipokula utakufa, lazima niwaambie ukweli” – RAIS MAGUFULI…Full video bonyeza play hapa chini kuitazama!