Watu 8 wamefariki dunia kutoka kwenye familia 6 Mkoa wa kusini Pemba huko kisiwa Panza kwa kudaiwa ni ulaji wa Samaki aina ya kasa kwanzia jana na wengine 34 walipatiwa matibabu
Inadaiwa watu hao waliokula kasa walianza kupata matokeo ya kuumwa na tumbo kwanzia siku chache ,walioathirika na ulaaji huo na kupelekea kupata Dalili za Kulegea mwili ,kutapika, kuharisha na tumbo kuuma hadi kupelekea vifo 8 kwa watoto chini ya miaka 10
Akizungumz na muandishi wa ayo tv kw njia simu Mkuu wa Mkoa wa Kusini pemba Mhe. Mattar Zahor amesema Sampuli za Vikohozi na Damu zimepelekwa kwa Mkemia mkuu kutambua ni kilichosababisha vifo hivyo ambavyo wananchi wamekua wakisema ni ulaaji wa kasa