Hizi hapa chini ni habari zote kubwa ambazo nimezikusanya kutoka kwenye Magazeti ya Tanzania leo July 8, 2017 ambazo zimepewa uzito wa juu na unaweza kuzipitia moja baada ya nyingine hapa kwenye millardayo.com.
Mkurugenzi wa zamani H'shauri ya Wilaya Geita Dan Mollel amefungwa kifungo cha nje miezi 12 kwa kutumia vibaya madaraka na rushwa #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
"Njia rahisi ya kumuangamiza kiongozi mdogo au mkubwa ni kumsifia hata pale anapokuwa amekosea…" – Nikki wa Pili. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
CHADEMA Arusha kimempitisha aliyekuwa Naibu Meya wa jiji la Arusha Viola Likindikoki kugombea nafasi hiyo kwa kipindi cha pili. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Mfanyabiashara Yusuf Manji ameondolewa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kupelekwa Keko akiwa chini ya ulinzi mkali. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Imeelezwa kuwa 80% ya Watanzania wanaishi kwa hofu ya kupoteza maeneo na kubomolewa makazi yao kutokana na kujenga kiholela. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Halmashauri ya Mji wa Kibaha itawatoza faini ya Tsh. 50,000 wafanyabiashara watakaokaidi na kufanya biashara stand ya Maili Moja. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
TRA Arusha imewataka wafanyabiashara na wamiliki wa bar na nyumba za wageni kutumia mashine za EFD ili kuepuka faini ya Tsh. 3m. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Mahakama ya Wilaya Serengeti imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela watu watatu waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya ujangili. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Jeshi la Polisi Tabora linawashikilia watu watatu akiwemo mwanamke mmoja mkazi wa Lufwiisi, Sikonge anayedaiwa kumuua mumewe. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatarajia kutangaza sifa na vigezo vitakavyotumika kupanga mikopo 2017/18. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Jeshi la Polisi Geita, limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya viongozi na wafuasi wa CHADEMA waliokuwa kwenye mkutano wa ndani. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Wananchi wa vijiji vya Saza na Mbagala, Songwe wameilalamikia kampuni ya Shanta Mine kwa kuziba njia za maji ktk Mto Lwika. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Waganga wa tiba asili Uyui, Tabora wamelalamika Polisi kuwakamata bila makosa licha ya kuwa na vibali vya kufanya kazi hiyo. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Wananchi 25,000 waliopimiwa viwanja Dodoma na kupewa hati ya kumiliki kwa miaka 33 wanabadilishiwa na kupewa za miaka 99. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Polisi DSM imeendelea kumshikilia Mbunge wa Kawe, Halima Mdee licha ya kumalizika kwa saa 48 zilizotolewa na DC Ally Hapi. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Wananchi wa Babati wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo baada ya kulazimika kuamka usiku wa manane kutafuta huduma ya maji. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) limeipiga faini ya Tsh. 25m Jiji la DSM kwa uchafuzi wa mazingira. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Imeelezwa kuwa uelewa mdogo juu ya matumizi sahihi ya dawa ni chanzo cha watu kukumbwa na matatizo kiafya wakati wazitumiapo. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Ustaadh Mesha Hamad mkazi wa Chanji anashikiliwa na Polisi Rukwa akituhumiwa kuwaficha watoto wanne kwa madai ya kuwafundisha dini. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Jeshi la Polisi Wilaya ya Chato, Geita linawashikilia viongozi watatu wa CHADEMA kwa madai ya kufanya mkusanyiko bila kibali. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Bei za dawa, vifaa vya tiba na vitendanishi vya maabara imeshuka kwa wastani wa 15%-80% baada ya MSD kununua dawa kwa wazalishaji. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema hatma ya mapacha walioungana ya ama kufanyiwa upasuaji au la itajulikana wiki ijayo. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
M/kiti UDP, John Cheyo amesema Mawaziri Wakuu wa zamani Lowassa, Sumaye wanatumia Dini na Katiba kuchonganisha wananchi na Serikali. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Polisi Kagera limewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kujihusisha na uchomaji moto nyumba 14 za wananchi wa kijiji cha Bugasha. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 8, 2017
Mkurugenzi wa Jiji DSM atozwa faini ya Tsh. 25m…ilipwe ndani ya siku 14…kisa kimeelezwa kwenye VIDEO hii hapa chini, bonyeza PLAY kutazama!!!
Serikali imetangaza GOOD NEWS kwa Watanzania baada ya Bohari ya Dawa ‘MSD’ kuanza kutekeleza agizo la Rais JPM kuhusu kununua dawa moja kwa moja kwa watengenezaji badala ya kwa wafanyabiashara na watu wa kati…VIDEO hii ina kila kitu, bonyeza PLAY kutazama!!!