Askari wawili wa kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani wameuawa na majambazi ambao idadi yao haijafahamika ambao baada ya kufanya mauaji walipora bunduki tano, risasi 60 na mabomu mawili ya machozi ndani ya kituo cha Polisi.
“Walikuwa ni majambazi wengi, walivamia na kuanza kuwashambulia askari wetu, walifanikiwa kuwaua askari wetu wawili na kuchukua silaha… Polisi imelaani tukio hilo, msako mkali umeanza na milioni 20 itatolewa kwa atakaefanikisha Majambazi hawa kukamatwa“– Advera Bulimba, msemaji wa Jeshi la Polisi akiongea on ITV
Majambazi hawa walivamia wakiwa na silaha za moto, mabomu ya kurusha kwa mkono na mapanga ambapo hili linakuwa tukio jingine kulisikia baada ya lile la Majambazi kufanya vivyo hivyo kwa kituo cha Polisi Geita.
Nakuhakikishia kukufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook