Leo August 26, 2019 Wakati bado Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya zaidi ya Watu 100 kufuatia ajali ya moto Morogoro ya lori la mafuta, baadhi ya Wananchi wa Kagera wamejitokeza kwa wingi kuchukua mafuta kwenye ajali ya Lori la mafuta lililoanguka jana eneo la Benako Ngara Mkoani Kagera.
Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ameongea na millardayo.com na AyoTV na kusema ameagiza Polisi kufanya msako na kuwakamata wote waliochota mafuta na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.