“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya ajali ya basi la abiria la kampuni ya Igunga Trans iliyosababisha vifo vya vijana wetu 11 JKT , askari 1 wa JWTZ na dereva waliopoteza maisha leo June 14, 2018 majira ya mchana katika mteremko wa Mwansekwa uliopo Mjini Mbeya.” Rais Magufuli
“Vijana wetu wamefariki dunia wakiwa safarini kutoka Tabora kwenda Kikosi cha JKT Itende Mbeya kwa ajili ya kuendelea na mafunzo ya JKT, tumewapoteza vijana shupavu waliojitolea kulijenga na kulipigania Taifa,” Rais Magufuli
“Nimeumizwa sana na vifo vya vijana hawa na nawapa pole Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jen. Venance Salvatory Mabeyo, Mkuu wa JKT Mej Jen. Martin Busungu, familia za marehemu na wote walioguswa na msiba huu” Rais Magufuli
Hizi ni salamu za rambirambi za Rais Magufuli alizozituma kupitia kwa RC Mbeya Amos Makalla kufuatia vifo vya watu 13 wakiwemo vijana 11 wa JKT waliokuwa wakisafiri kutoka Tabora kwenda Mbeya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kisha kupinduka katika eneo la Mwansekwa, Mjini Mbeya.
Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, na amewaombea majeruhi wote 25 wa ajali hiyo wapone haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na majukumu ya kila siku.
BREAKING: Ajali ilivyoua Askari 10 wa JKT, 200 wamejeruhiwa muda huu Mbeya