Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ‘UVCCM’ Mkoa wa Arusha na Diwani wa Kata ya Sambasha, Lengai Sabaya leo August 11, 2017 amefikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka mawili; kujifanya Mtumishi wa Usalama wa Taifa na kughushi kitambulisho cha Usalama wa Taifa na kukitumia kutapeli.
Mshtakiwa ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti kwa kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya Tsh. Milioni 3 kila mmoja na kesi imeahirishwa hadi August 30, 2017.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, L. Sabaya amesema amerudishwa mara ya nne Mahakamani na kusomewa makosa yale yale. #MillardAyoUPDATES. pic.twitter.com/PmEWHr5r0t
— millardayo (@millardayo) August 11, 2017
ULIPITWA? Kiongozi UVCCM Mahakamani kwa kutumia kitambulisho feki cha Usalama wa Taifa…tazama kwenye video hii chini!!!