Kesi ya kusambaza picha za ngono kupitia mtandao wa Instagram inayomkabili msanii Wema Sepetu imefikisha siku 42, huku upelelezi ukiwa haujakamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kesi hiyo ilipangwa leo kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde ambapo Wakili wa Serikali Mosia Kaima amedai upelelezi haujakamilika.
Wakili Kaima ameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Kasonde amesema kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika kesi hiyo itatajwa tena January 28, 2019.
Wema alifikishwa mahakamani hapo November mosi, 2018 akikabiliwa na makosa ya kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika ukurasa wake wa Instagram, October 15, 2018 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam.