Club ya Juventus ya Italia tayari imekamilisha usajili wa kumsajili staa wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo kwa mkataba wa miaka minne, Ronaldo kasajiliwa kwa dau la euro milioni 100 kutoka Real Madrid kwenda Juventus.
Kwa mujibu wa mtandao wa SportsBible.com unaeleza kuwa saa 24 baada ya Ronaldo kutangazwa kusajiliwa na Juventus, zimeuzwa jumla ya jezi zake 520000 kupitia mtandaoni na kwenye maduka ya uuzaji jezi ya Juventus na Adidas ambao ndio watengenezaji wa jezi hizo.
Jezi moja ya Ronaldo inauzwa euro 105 ambazo ni zaidi ya Tsh 270,000 hivyo ukizidisha mara 520000 , Ronaldo atakuwa ameiingizia Juventus kwa mauzo ya jezi pekee ndani ya saa 24 toka asajiliwe jumla ya euro milioni 54.6 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 144.
Haji Manara kaeleza sababu za kuwasajili Wawa, Dida na Kagere