Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Wanamaji kimefanya Oparesheni katika Bahari ya Hindi na kukamata wahalifu wanaotumia zana haramu za uvuvi pamoja na wavuvi haramu.
Kamanda wa Polisi Makao Makuu ya Wanamaji (T) ACP Evance Mwijage amewaambia waandishi wa habari kuwa katika oparesheni hiyo wamefanikiwa kumkamata mkazi wa Kisiwa cha Kwale Hamad Omary ambapo alikutwa na mazao ya baharini bila kibali.
Pia Kamanda ACP Mwijage amesema katika Kisiwa cha Fungu Mbaraka wilaya ya Mafia wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili Othman Fakhi na Mbwana Fakhi wakiwa kwenye boti wakiwa na zana haramu zenye macho MM 10 ya urefu wa mita 200, mitungi ya gesi 12, viatu vya kuogolea na miwani ya kuzamia.
“Pia tumekamata watuhumiwa 43 katika boti maarufu ya Mv Chalanga wakivua samaki bila leseni katika eneo la Kisiwa cha Fungu Mbaraka wilaya ya Mafia, lakini wamepigishwa faini ya Shilingi Milioni 4.3″amesema.