Serikali kupitia wakala wa ufundi na umeme Temesa inaendelea na matengenezo ya vivuko vipya 8 kwa mikataba yenye thamani ya bill 33.2 huku ikikarabati vivuko 14 kwa mikataba ya thahamani ya bill 22. 99.
Hayo yamebainishwa na naibu katibu mkuu wizara ya ujenzi na uchukuzi LUDOVICK NDUHIYE wakati wa uzinduzi wa kivuko cha Mv Tanga ambapo amesema serikali imedhamiria kuondoa changamoto ya vivuko kwenye maeneo mbali mbali nchini.