Naibu Spika Dr. Tulia Ackson aliongoza Wananchi wa Mbeya pamoja na Washiriki wa tamasha la ngoma za asili la Tulia Traditional Dances Festival 2018 kusimama kwa dakika moja ili kuomboleza tukio la msiba uliotokea katika kivuko cha MV Nyerere mkoani Mwanza kilichozama katika ziwa Victoria mkoani Mwanza kilichokuwa kikifanya safari zake kati ya Bugorola na Kisiwa cha Ukerewe.
“Nitoe pole sana kwa msiba huu uliotupata, msiba huu ni mkubwa sana kwa taifa letu na tunachoweza kusema ni kwamba ndugu zetu wametangulia mbele za haki na tuwaombee majeruhi waweze kureja katika hali zao za kawaida” –Dr. Tulia Ackson
BREAKING: Tazama Fundi Mkuu wa MV. Nyerere ameokolewa akiwa HAI