Tanzania imepata msiba mwingine mkubwa baada ya mafuriko yaliyotokana na mvua ya mawe iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi na kusababisha vifo na wengine wakajeruhiwa kwenye wilaya ya Kahama Shinyanga.
Mpaka March 5 2015 serikali ilithibitisha kwamba waliofariki wamefikia 45 ambapo waliojeruhiwa walikua wanaendelea kupatiwa matibabu huku mkurugenzi Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Nyanchenghe Nanai akisema ni zaidi ya watu 70 hawana makazi na nyumba zilizoharibiwa ni 137.
Hiyo imeilazimu serikali kupeleka msaada wa haraka ili kuwanusuru waathirika wa mafuriko hayo ambapo pia Waziri mkuu amekwenda kuwapa pole na bado mkurugenzi huyu amesema bado misaada inahitajika kwa ajili ya waathirika sanasana ya makazi na chakula.
Watu 574 hawana sehemu ya kuishi ambapo waliojeruhiwa ni 82, watu waliokosa makazi wanaishi kwenye shule za msingi Mwakata, Numbi na Mwaguguma ambazo imebidi zifungwe kwa muda kutoa huduma za masomo.
Kama una chochote ungependa kukifikisha kwa walioathirika na haya maafuriko iwe ni pesa au nguo au chakula ungana na wengine kwenye hii account ya twitter kwa kubonyeza hapa >>> DAR FLOODS