Mbunge wa Geita Joseph Musukuma ameilalamikia Serikali ikiwemo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushindwa kutoa msaada kwa wasanii wa nchini na badala yake imekuwa ikiishia kuwafungia kazi zao kwa madai ya kukiuka maadili.
Musukuma amesema…>>>“Kinachomfanya mtu ahamasike kwenda kwenye mziki ni pamoja na matangazo mazuri atakayotangaza msanii lakini kinachofanywa sasa msanii anafanya kazi nzuri kwenye kushuti akikosea kidogo kwenye mpasuo Waziri huyo amefunga…Mimi nauliza unafungia wasanii wa Tanzania kuonesha mpasuo, embu angalia miziki ya kina Rihanna na mnakaa kuangalia kwenye Youtube kila saa ila ya Tanzania mnataka avae dela”
Dakika 5 za Mbunge Shangazi Bungeni “Zichukuliwe hatua za haraka”