Mbunge wa Sumbawanga mjini Aeshi Hilaly amesema katika sehemu Serikali ilifanya makosa makubwa ni kuwazuia wafanyabiashara wa zao la mahindi kuuza nje ya nchi hatua iliyosababisha hasara kwa wakulima, Aeshi amezungumza hayo wakati akichangia mapendekezo yake katika makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/19
“Nikupongeze Waziri kwa kutoa kikwazo cha vibari cha kusafirisha mahindi nje ya nchi, tusifanye tena makosa kama haya. Mahindi ndio zao kuu la chakula na biashara leo hii gunia moja la mahindi ni shilingi elfu 15 embu niambie mkulima huyu leo hii akalime tena mahindi ataweza? Na kwa kahati mbaya mnambana kila kona” –Aeshi Hilaly
Hakimu aeleza sababu za kukataa kujitoa kesi ya Nondo