Serikali kupitia kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na Ajira Anthony Mavunde imeanzisha mpango mpya wa kuwasaidia vijana wanaomaliza masomo na kukutana na kikwazo cha kupata kazi kwa kigezo cha kutakiwa kuwa na uzoefu kazini. Mavunde amelieleza bunge wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum CCM Zainab Katimba aliyehoji Serikali inamkakati gani wa kuwasaidia vijana wanaomaliza vyuo na kukosa ajira kwa kigezo cha kutokuwa na uzoefu kazini.
“Kumekuwepo na changamoto kubwa katika masuala ya uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi, Asilimia kubw aya vijana wanaomaliza vyuo vikuu wamekuwa wakipata tabu sana na tumehakikisha tunatengeneza mwongozo kati ya Serikali, waajiri na vyama vya wafanyakazi ili vijana hawa wakimaliza mafunzo yao tunawapeleka moja kwa moja katika makampuni wakajifunze kazi ili kuwasaidia katika kikwazo cha uzoefu ” –Mavunde
Maamuzi ya IGP Sirro kwa RPC wa ‘Shambulio la Aibu, kujikoolesha’