Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, ameagiza waajiri ambao hawajajisajili na mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi kufanya hivyo, vinginevyo wafikishwe mahakamani mara moja.
Taarifa zinaonyesha kuwa jiji la Mwanza lina waajiri 1228, lakini kati ya hao ni waajiri ni 482 tu ndio waliojisajili na mfuko huku waajiri wengine 746 wakiwa bado hawajajisajili.
” Mwaajiri usipojiunga na Mfuko wa Fidia kwa mfanyakazi, faini Milioni 50, Jela miaka 6″ -Mavunde